Ufini

Eneo na Idadi ya Watu

Ufini inapatikana Kaskazini mwa dunia na iko baina ya Uswidi na Urusi. Upande wa Kaskazini, Ufini inapakana na Norwe ...

Serikali na Manispaa

Ufini ilipata uhuru tahere 6 Desemba mwaka 1917. Kabla ya Uhuru, Ufini ilikuwa chini ya utawala wa Urusi kati ya mwaka ...

Vyanzo vya Kazi

Sekta ya misitu ni chanzo muhimu cha kazi nchini Ufini na imekuwa chanzo kikubwa cha kazi katika historia ya Ufini. ...

Kuishi Ufini kama Mhamiaji

Kuna haki na majukumu sawa kwa wahamiaji sawa na Wafini. Wahamiaji wana haki ya kuabudu katika dini zao na ...

Mahusiano katika Familia

Wanawake na wanaume wanachukuliwa kuwa sawa nchini Ufini. Karibu asilimia 50 ya wajumbe wa Bunge na wafanyakazi ...

Tabia za Kitamaduni

Kusalimia kwa mikono na kutikisa kichwa ndizo njia za kusalimia nchini Ufini. Marafiki wa karibu au jamaa wanaweza ...

Tabia ya Nchi

Ufini ina aina nne za majira tofauti: machipuko, majira ya joto, mapukutiko na majira ya baridi. Kiwango cha joto hubadilika ...




Eneo na Idadi ya Watu

Ufini inapatikana Kaskazini mwa dunia na iko baina ya Uswidi na Urusi. Upande wa Kaskazini, Ufini inapakana na Norwe. Upande wa Kusini Ufini inapakana na Estonia. Lugha rasmi nchini Ufini ni Kifini na Kiswidi. Idadi ya watu nchini Ufini ni takribani watu milioni 5.5. Kuna takribani watu 200 000 wanaozungumza kugha za kigeni nchini.

Sheria ya Ufini inatoa uhuru wa kuabudu. Dini iliyoenea sana ni ya Kikristo. Kanisa kubwa ni la kanisa la Kiinjilisti la Walutherani ambalo takribani asilimia 80 ya watu huabudu, na linalofuata kwa ukubwa ni kanisa la Othodoksi lenye asilimia 1 ya watu. Kuna maelfu ya Waisilamu nchini Ufini. Madhehebu mengine yanayopatikana nchini Ufini ni Mashahidi wa Yehova, Kanisa Huru la Ufini, Kanisa la Katoliki na Kanisa la Wasabato la Ufini.

Serikali na Manispaa

Ufini ilipata uhuru tahere 6 Desemba mwaka 1917. Kabla ya Uhuru, Ufini ilikuwa chini ya utawala wa Urusi kati ya mwaka 1809–1917, ingawa Ufini ilijiamulia mambo yake. Kabla ya hapo, Ufini ilikuwa sehemu ya Uswidi kwa kipindi cha miaka 600.

Ufini ni jamhuri ya kidemokrasia. Kiongozi wa serikali ni Rais, ambaye anachaguliwa kwa uchaguzi mkuu unaofanyika kila baada ya miaka sita. Rais anaweza kuchaguliwa kutawala awamu mbili zinazofuatana.

Nchini Ufini, wanaume na wanawake wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi wana haki ya kupiga kura. Wanawake walipata haki ya kupiga kura mwaka 1906, kama taifa la kwanza kuwapa wanawake haki ya kupiga kura. Nchini Ufini kuna mfumo wa vyama vingi na hivi sasa kuna vyama vinane.

Bunge la Ufini huunda sheria na kupitisha bajeti ya serikali. Kuna wajumbe 200 Bungeni. Wajumbe huchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu. Serikali huandaa na kutekeleza maamuzi yanayopitishwa na Bunge. Serikali inaundwa na Waziri Mkuu na mawaziri wote.

Ufini imegawanya katika manispaa yanayojitegemea. Manispaa haya yana mamlaka ya kukusanya kodi kutoka kwa wakazi wake na kupitisha bajeti. Manispaa yana jukumu la kutoa huduma kwa wakazi wake, kama vile huduma za afya na ustawi wa jamii na elimu ya msingi.

Vyanzo vya Kazi

Sekta ya misitu ni chanzo muhimu cha kazi nchini Ufini na imekuwa chanzo kikubwa cha kazi katika historia ya Ufini. Sehemu kubwa ya Ufini ni misitu. Misitu imepata umaarufu na kuitwa Dhahabu ya Kijani ya Ufini. Bado kilimo ni chanzo kikubwa cha ajira, lakini kwa sababu ya kutumia teknolojia ya kisasa inatoa ajira kwa Wafini wachache tu.

Ufini ilikuwa nchi ya viwanda miaka ya 1950. Kukua kwa viwanda kuliiwezesha Ufini iwe sehemu ya ukuaji wa uchumi wa Ulaya. Baadhi ya viwanda muhimu ni kujenga meli na viwanda vya misitu. Kwa kipindi cha miongo iliyopita teknolojia imekuwa sehemu muhimu ya viwanda, na miaka ya hivi karibuni, sekta ya michezo imepata umaarufu. Waajiri wakubwa nchini Ufini ni teknolojia na huduma zinazohusu teknolojia.

Kuishi Ufini kama Mhamiaji

Kuna haki na majukumu sawa kwa wahamiaji sawa na Wafini. Wahamiaji wana haki ya kuabudu katika dini zao na kusherehekea siku kuu zao na dini zao. Wahamiaji wameanzisha makundi yao ya dini na sehemu za kuabudu kote nchini Ufini. Mwelekeo wa Wafini kuhusu wahamiaji haubagui. Kuna matukio ya kupinga lakini ubaguzi ni marufuku kwa mujibu wa sheria ya Ufini.


Mahusiano katika Familia

Wanawake na wanaume wanachukuliwa kuwa sawa nchini Ufini. Karibu asilimia 50 ya wajumbe wa Bunge na wafanyakazi Serikalini ni wanawake. Wanawake wengi hufanya kazi mbali na nyumbani na wanaume hushiriki katika kazi za ndani na kulea watoto. Ukatili dhidi ya wanawake ni kosa la jinai sawa na ukatili dhidi ya watu wengine nyumbani au sehemu nyingine yoyote.

Nafasi ya mtoto nchini Ufini ni nzuri. Maslahi ya mtoto yanazingatiwa hata kabla ya kuzaliwa katika kliniki za wajawazito. Huwezi kumpiga mtoto wala kumvuta kwa nywele zake. Ufini ina mfumo mzuri wa shule za chekechea, na watoto wote kati ya miaka 7 hadi 16 husoma shule za msingi na sekondari.

Tabia za Kitamaduni

Kusalimia kwa mikono na kutikisa kichwa ndizo njia za kusalimia nchini Ufini. Marafiki wa karibu au jamaa wanaweza kusalimia kwa kukumbatiana. Kwa kawaida katika majiji makubwa watu husalimia watu wanaowafahamu pekee. Watu hutazamana machoni wanaposalimiana.

Wafini huwa waangalifu wanapoanza kuzungumza na mtu wasiyemjua. Kwa sababu hii, Wafini wanachukuliwa kuwa wanaona aibu na fidhuli. Kwa kawaida huwa hawaombi kuzungumza sana katika mijadala ya hadharani na hueleza hoja moja kwa moja.

Usawa na Haki ni vitu muhimu katika maisha ya Wafini. Aidha Wafini wanapenda ukweli na kutimiza ahadi. Wafini wanapenda sana kufanya kazi kwa bidii. Kutunza muda na kufika kwa muda ni muhimu sana.

Wafini wengi hunywa pombe kwa wingi wakati wa wikendi na siku kuu maalum hali ambayo inaweza kuwakanganya wahamiaji. Kulewa kupita kiasi husababisha magonjwa na migogoro katika familia.

Tabia ya Nchi

Ufini ina aina nne za majira tofauti: machipuko, majira ya joto, mapukutiko na majira ya baridi. Kiwango cha joto hubadilika sana katika majira haya. Hali ya hewa hutofautiana katika sehemu mbalimbali za nchi. Kaskazini mwa Ufini ni baridi zaidi ya Kusini mwa Ufini.

Machipuko

Msimu wa Machipuko huanza mwezi Machi hadi mwezi Mei. Wakati wa machipuko barafu huyeyuka. Mimea huchipuka. Matawi huota kwenye miti na miti huanza kukua. Watu huanza kutoka nje sana na kuna mwanga wa jua wa kutosha.

Majira ya Joto

Miezi ya majira ya joto ni Juni, Julai na Agosti. Mwezi wa joto kali ni Julai. Wakati wa majira ya joto kuna mwanga jioni na usiku. Jua hutua usiku wa manane na kuchomoza mapema. Wakati wa majira ya joto Wafini hutumia muda mwingi kukaa pamoja nje. Maisha huwa ya kuchangamsha na watu huwa wazi zaidi. Majira ya joto ni majira ya likizo pia.

Mapukutiko

Majira ya mapukutiko huanza Septemba hadi Novemba. Mapukutiko huwa na baridi kali na mvua nyingi. Matawi ya miti hupukutika. Siku huwa fupi na hali ya hewa huwa ya baridi kali na watu hujiandaa kwa kununua nguo za baridi. Wakati wa mapukutiko watu hujishughulisha na kazi, kusoma na mambo wanayoyapenda.

Majira ya Baridi

Nchini Ufini miezi ya Desemba, Januari, na Februari ni miezi ya baridi. Wakati wa majira ya baridi kuna barafu nyingi na ardhi huwa imefunikwa na barafu. Mwezi wa baridi kali ni mwezi wa Februari. Ili ustahimili majira ya baridi lazima uvae nguo za baridi na ujifunze kuvaa nguo nyingi. Kwa sababu ya hali ya baridi kali watu hupendelea kukaa ndani lakini maisha huwa ya kawaida.

Pakua hapa yaliyomo katika kurasa huu katika muundo wa PDF.