Kujiandaa Kuhama

Maandalizi ya Kuhama Kabisa

Wewe ukiwa mhamiaji halali pamoja na wale waliojumuishwa mmepewa hadhi ya mhamiaji, kibali cha kudumu ...

Hati za Kusafiri

Hakikisha umebeba hati za kusafiri na hati nyingine za kukutambulisha. Hati za asili zitasaidia katika mchakato wa ...

Vyeti vya Shule na Kazi

Katika hatua za awali za kutathmini hitaji la elimu na mafunzo wahamiaji wataombwa kuwasilisha vyeti vyao vya shule ...

Mpango wa Elimu na Kutafuta Ajira

Ili mhamiaji apate ajira, mara nyingi hupewa mafunzo na elimu ya ziada nchini Ufini. Ili kuhakikisha kwamba unapata elimu ...

Dawa Uliyoagizwa Kutumia na Daktari

Katika mahojiano utakayofanyiwa na muuguzi mtapitia magonjwa ambayo umewahi kuugua, dawa ulizotumia na chanjo ...

Kujiandaa Kisaikolojia Kuhusu Safari

Ni muhimu kwa mhamiaji kujiandaa kisaikolojia kwa fursa na changamoto atakazopata katika makazi yake mapya yeye ...




Maandalizi ya Kuhama Kabisa

Wewe ukiwa mhamiaji halali pamoja na wale waliojumuishwa mmepewa hadhi ya mhamiaji, kibali cha kudumu cha kuishi na haki ya kufanya kazi nchini Ufini. Ni muhimu ujadiliane na familia yako kuhusu uwezekano wa kuhama kabisa na fasili yake, ni vizuri kupanga safari hii pamoja. Unakaribishwa katika makazi mapya, watu wapya wenye utamaduni na tabia tofauti ambao watawasiliana na wewe katika lugha ngeni.


Hati za Kusafiri

Hakikisha umebeba hati za kusafiri na hati nyingine za kukutambulisha. Hati za asili zitasaidia katika mchakato wa usajili na katika hati mpya za kusafiri.


Vyeti vya Shule na Kazi

Katika hatua za awali za kutathmini hitaji la elimu na mafunzo wahamiaji wataombwa kuwasilisha vyeti vyao vya shule na vinavyohusu kazi walizofanya. Kwa huvyo, ni muhimu ubebe vyeti vyako vyote vya elimu, shahada na stakabadhi za kazi. Itakuwa vizuri ukithibitisha kwamba vyeti hivyo ni halali na ikiwezekana vitafsiriwe katika Kiingereza na viidhinishwe na katika nchi yako.

Ni muhimu pia kuwa na vyeti kwa sababu shahada, elimu na uzoefu wa kazi uliopata nje ya Ufini vinaweza kukusaidia unapofanya mipango ya kusoma nchini Ufini. Stakabadhi za kazi uliofanya zitakusaidia kupata kazi.

Mpango wa Elimu na Kutafuta Ajira

Ili mhamiaji apate ajira, mara nyingi hupewa mafunzo na elimu ya ziada nchini Ufini. Ili kuhakikisha kwamba unapata elimu inayofaa nchini Ufini lazima tayari uwe na mpango wa kusoma na kufanya kazi sehemu unayoishi. Hakikisha katika mpango wako unaweka wazi mahali, uliposoma, mwaka na taaluma uliyoisomea, shahada ulizopata na ulikofanya kazi. Kumbuka kuandika ujuzi wako maalum katika mpango wako na unapaswa kufanya kazi gani. Aidha ni muhimu kuandaa wasifukazi (Curriculum Vitae) unaoonyesha ujuzi na uzoefu wako. Unaweza kupata vidokezo vya kuandaa wasifukazi kwenye mtandao.

Mara baada ya Kuhamia nchini Ufini watoto watapelekwa shuleni ambako watapata mafunzo ya elimu ya msingi. Wazazi wanahimizwa kuwaandaa kisaikolojia kuhusu mazingira ya shule mpya. Kipeperushi hiki kinatoa taarifa ya msingi kuhusu shuke na unaweza kupata taarifa kuhusu shule za Ufini kupitia tovuti nyingine (angalia viungo muhimu vya intaneti).

Dawa Uliyoagizwa Kutumia na Daktari

Katika mahojiano utakayofanyiwa na muuguzi mtapitia magonjwa ambayo umewahi kuugua, dawa ulizotumia na chanjo ulizopata. Kwa hivyo, unapokuwa ukisafiri kumbuka kubeba stakabadhi za matibabu na nyaraka za daktari na ikiwezekana kadi za chanjo. Stakabadhi hizi zitaharakisha mchakato wa kupata matibabu na dawa sahihi katika manispaa yako mapya unayoishi. Hakikisha unabeba dawa zako za lazima zinazotosha mwezi mzima.


Kujiandaa Kisaikolojia Kuhusu Safari

Ni muhimu kwa mhamiaji kujiandaa kisaikolojia kwa fursa na changamoto atakazopata katika makazi yake mapya yeye na familia yake.

Kuanza maisha katika nchi mpya ni fursa ya kujifunza mambo mapya, kufanikiwa na kuimarika. Mwanzoni familia yote italazimika kujifunza na kuzoea mambo mapya. Watoto huenda shuleni huku wazazi wakipata mafunzo ya kutangamana na jamii. Kila mmoja anajifunza lugha ya Kifini. Familia inapata fursa ya kufahamu watu na mazingira yao.

Mazingira mapya yana athari tofauti kwa kila mmoja na yanaweza kuleta mabadiliko ya majukumu katika familia. Familia yote lazima ijifunze lugha na tabia mpya. Kwa kawaida watoto hujifunza lugha ngeni haraka kuliko wazazi wao. Kuna uwezekano kwamba watoto watapata urahisi wa kumudu mazingira ya nje kuliko wazazi wao. Hali hii inaweza kuathiri majukumu ya watoto katika familia.

Nchini Ufini wanawake wanaelimishwa na kufanya kazi mbali na nyumbani. Elimu na ajira kwa mwanamke mhamiaji inaweza kubadilisha majukumu ambayo awali walikuwa wanayatekeleza katika familia. Huenda wazazi wasimudu jukumu la kuwasaidia watoto kutokana na changamoto zinazowakabili kama wazazi. Unaweza kumweleza kwa mfano afisa wa ustawi kwa siri hali ya familia yako. Kukiri kuwepo kwa tatizo na kulijadili na mtu ambaye si wa familia kunaweza kusaidia kupata ufumbuzi wa matatizo yanayosababishwa na mabadiliko.

Ni muhimu kukumbuka kwamba kutangamana na utamaduni mpya kunaweza kusababisha mabadiliko mabaya ya hali mbaya ya usununu. Aidha inavutia sana kuishi katika nchi ya Ufini ambayo ina usalama. Wakati mwingine kutokuwepo kwa familia ya mhamiaji, aina mpya ya maisha, maadili na dini tofauti vinaweza kusababisha upweke na kutamani nyumbani. Unaweza kujadili hali ya usununu inayotokana na kutangamana na muuguzi, daktari au afisa wa ustawi kwa siri. Aidha wahamiaji wengine unaowafahamu wanaweza kukusaidia kuelezea hisia na hali hii. Hisia hazifichiki lakini kuwa wazi kuhusu hisia hizo kunaweza kusaidia kuelewa hali inayokukabili.

Mhamiaji atahitajika kufanya kazi kwa bidii sana Ili atimize malengo yake katika mazingira mapya. Unaweza kufikia ndoto zako iwapo mikakati ya elimu na ajira inatekelezeka. Unaweza kupata usaidizi kuhusu mikakati hii kutoka kwa mshauri wa ajira na afisa wa ustawi wa jamii.

Pakua hapa yaliyomo katika kurasa huu katika muundo wa PDF.